Thursday, 1 March 2018

Mshauri wa Trump na mkurugenzi wa mawasiliano ajiuzulu

  Bi Hicks

MKURUGENZI wa mawasiliano na mmoja wa washauri wa karibu wa muda mrefu wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Hicks ameachia ngazi.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29, aliyekuwa mwana mitindo na mfanyakazi wa kampuni ya Trump, amekuwa karibu naye kwa miaka mingi.

Anaripotiwa kuwaambia wafanyakzai wenzake kuwa amehisi ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House.

Yeye ni mtu wa nne aliyeshika wadhifa wa mkurugenzi wa mawasiliano. Msemaji wa White House, Sarah Sanders amesema haijulikani ni lini haswa Hicks ataondoka.

Amekanusha kuwa hatua hiyo inahusiana na ushahidi ambao Hicks aliutoa mbele ya kamati Congress wakati aliporipotiwa kukiri kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Trump.


Wakati wa kampeni za uchaguzi, Hick alifanya kazi kama katibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi ya kuongoza idara ya mawasiliano ya White House, Agosti mwaka uliopita, baada ya ufutaji kazi wa ghafla wa Anthony Scaramucci. Kabla yake, Sean Spicer na Mike Dubke walishika wadhifa huo.

No comments:

Post a Comment