Wednesday, 14 March 2018

Mwalimu aliyefundisha komputa ubaoni aula


MWALIMU Owura Kwadwo ambaye mwezi uliopita aliweka picha yake mtandaoni akichora programu ya Microsoft Word kwenye ubao wakati wa darasa la tarakilishi, sasa anahudhuria mkutano wa waelimishaji wa Microsoft unaofanyikia nchini Singapore.
Picha hiyo ilivuma sana mitandaoni.  Iligundulika kuwa alifanya hivyo kwa sababu shule anayofundishia haikuwa na tarakilishi za kuwafundushia wanafunzi somo hilo la kompyuta.
Alisema "kufundisha somo la kompyuta nchini Ghana inachekesha. Ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, "Nimefika nchini Singapore katika mkutano wa Microsoft Global Education Exchange, Ninatarajia kujifunza mengi. Asante Microsoft.
Baada ya picha yake Owura Kwadwo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, kampuni ya Microsoft ilivutiwa na mwalimu huyo na kumpatia msaada wa vifaa vya kumsaidia katika kazi yake.
Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment