Friday, 23 March 2018

Mwalimu wa sekondari mbaroni kwa kumwita Rais Magufuli dikteta


Augustine Ollomi

Khadija Rashid, Kagera

MWALIMU wa shule ya sekondari Nyakisasa, Deogratius Simon (34) anashilikiwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera, akituhumiwa kumkashifu, Rais Dk. John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amesema mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni dikteta anayeminya demokrasia.

Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya mwaka 2016 – 2018 kupitia mtandao wa kijamii ambapo inadaiwa alikuwa akisambaza ujumbe ambao polisi wanaona ulikuwa na lengo la kumchafua Rais Magufuli.

Shule ya sekondari Nyakisasa ipo katika wilaya ya Ngara, mkoani Kagera na kwamba kosa hilo ni matumizi mabaya ya mtandao.

Wakati huo huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara, Abed Maige amewaonya watu wasiopenda amani hapa nchini na hivyo kutumia mitandao ya kijamii kuivuruga waache mara moja kwa kuwa wanabainika sheria itachukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment