Wednesday, 21 March 2018

Mwanafunzi aliyechaguliwa kuwa DC akataa akihofia usama wake


Feisal Abdullahi Omar
MWANAFUNZI mwenye umri wa miaka 16 nchini Somalia amekataa uteuzi wa kuwa mkuu wa wilaya (DC), huko Kusini Mashariki mwa Hirshabelle.
Feisal Abdullahi Omar aliombwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mohamed Ali Adle. Amesema uteuzi huo ulikuja baada ya watu kumtembelea baba yake na kuwaomba kupendekeza mwakilishi katika ukoo wao.
“Nilipokuwa nikisubiri mkutano wa ukoo, nilipata barua ya uteuzi huo kutoka kwa waziri ambaye alimpatia baba yangu barua hiyo. Nilishangaa,”
Lakini amekataa uteuzi huo kwa kusema kwamba asingeweza majukumu ya nafasi hiyo ya uongozi.Ameongeza kuwa kuna changamoto kubwa katika ukanda au mkoa anamoishi kuhusiana na masuala ya usalama.
“Ninahofia usalama wangu mwenyewe ... Siwezi kuchukua jukumu hilo kwa sababu hali ya usalama katika nchi hii sio nzuri,”amesema.
Mji wa Gambole uko kilomita 50 (mita 31) Magharibi mwa Jowhar na unashikiliwa na wapiganaji wa kundi la al-Shabab linalohusishwa na al-Qaeda ambapo hivi karibuni makundi hayo yameongeza mashambulizi kwa askari wa serikali na Umoja wa Afrika.

No comments:

Post a Comment