Sunday, 4 March 2018

Mwanamume ajipiga risasi na kujiua nje ya White House


Polisi nje ya Ikulu ya White House

MWANAUME mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema
Kikosi hicho kimebainisha kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi. Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida.
Mwanamume huyo alikuwa kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na wale walioshuhudia.
Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.
Jina na mtu huyo bado halijatangazwa. Kumekuwa na visa kadha vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni.
Kisa cha hivi karibuni Februari 3, gari liliendeshwa kwenda kwenye kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa miaka 35 alikamatwa.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment