Monday, 12 March 2018

Mwenyekiti, mtendaji wa kijiji mbaroni kwa kuwakodisha wakimbizi


KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilayani Kakonko mkoani Kigoma inawashikilia mwenyekiti, ofisa mtendaji wa kijiji cha Kikurazo na Warundi watano kwa kosa la kuwakodisha wageni hao mashamba zaidi ya
hekari 100 mali ya kijiji hicho.

Wanashiliwa baada ya oparesheni iliyofanywa na kamati hiyo katika kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kukagua usalama wa mipaka ya Tanzania.

Akizungumzia operesheni hiyo , mkuu wa wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala amesema walifanikiwa kuwatia mbaroni washukiwa hao baadaa ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wependa maendeleo.

Ameongeza kuwa Warundi hao wanapofika kijijini hapo hukodishiwa maeneo hayo ambapo wamekutwa wamelima mihogo, mahindi na karanga wakati baadhi ya wananchi wanakosa maeneo ya kulima.

Amesema wao kama viongozi wa wilaya waliamua kwenda eneo hilo ambapo walikuta kuna mshamba zaidi ya hekari 100 zinazolimwa na Warundi kwa kukodishiwa na viongozi wa kijiji kwa gharama ya sh. 40000 hadi sh.60,000 kwa heka moja na kujipatia fedha hizo.

Pia amesena oparesheni hiyo ni muendelezo wa nyingine kwakuwa suala hilo linaweza kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na muingiliano wa mipaka.

No comments:

Post a Comment