Thursday, 15 March 2018

Mwigulu atembelea mahali patakapojengwa ofisi za uhamiajiWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba

Tunu Albert, Dodoma

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma mjini, ambapo panatarajiwa kujengwa ofisi za makao makuu ya Idara ya uhamiaji.
Tayari Rais Dk. John Magufuli, ameshatoa sh. bilioni 10 na kwamba ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Akizungumza wakati alipotembelea ofisi hizo leo, Dk Mwigulu amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapa fedha hizo.
 Amesema eneo hilo kubwa lenye mita za mraba 9,777 ndilo litakalotumika kujenga jengo hilo kubwa na la kisasa kwa ajili ya idara hiyo.
“Eneo limeshapatika kubwa na la kutosha ili kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo Rais amesema wakati anatuaidi kutupa fedha hizi, lipo karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa, zimamoto na ofisi nyingine za serikali,” ameongeza waziri Dk. Mwigulu.
Ametoa rai kwa Idara ya Uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwani kama wangesubiri fedha za bajeti ya wizara ingechukua muda mrefu kupatikana.
Naye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala amemshukuru Rais Dk. Magufuli kwa kuwapa fedha hizo kujenga jengo la kisasa na hadi sasa wameshapa eneo kubwa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote.

No comments:

Post a Comment