Saturday, 24 March 2018

Mwigulu awasili mlima Sekenge kushuhudia ajali ya gari la mafuta


Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akiangalia eneo ambalo gari hilo limeteketea kwa moto pamoja na watu wawili wakati linapanda mlima Sekenke mkoani Singida.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba amewasili eneo la tukio ilipotokea ajali ya moto baada ya roli la mafuta kulipuka kwenye mlima Sekenke na kusababisha vifo vya watu wawili.

Waziri Dk. Mwigulu amefika kuangalia jinsi ajali ya gari hilo la mafuta lilivyoanguka na kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu hao ambao wameungua kiasi cha kutotambuliwa hadi sasa huku jitihada za kuwatambua zikiendelea.

Kwa mujibu wa shuhuda Edward Lameck, 16, aliyekuwa anapita eneo hilo amesema breki za gari hilo ziligoma kusababisha matairi ya mbele kuanza kuwaka moto hali iliyosababisha gari hilo kutumbukia bondeni na kuteketea kwa moto.

No comments:

Post a Comment