Monday, 12 March 2018

Naibu katibu mkuu Bavicha ajiuzulu


ALIYEKUWA naibu Katibu mkuu Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema (Bavicha), Tanzania Bara, Getrude Ndibalema amejiuzuru nafasi hiyo.

Katika taarifa yake aliyoitoa leo amesema atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho.

“Kuanzia leo Machi 12 nautangazia umma wa Watanzania na wanachama wa Chadema kujiuzulu nafasi hii ya naibu Katibu mkuu wa Bavicha Tanzania Bara ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na kubaki mwanachama na Mtanzania wa kawaida ili niweze kufanya mambo yangu binafsi kulingana na taaluma yangu kwa uhuru zaidi,” amesema.
Getrude Ndibalema

No comments:

Post a Comment