Sunday, 4 March 2018

Nape aivalia njuga shule ya Litingi

Nape Nauye

SEKTA ya elimu imeimarika kwa kiwango cha kuridhisha katika kipindi cha muda wa zaidi ya miaka miwili cha utumishi wa mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nauye.

Nauye amesema amefanikiwa kufanya mabadiliko hayo katika kipindi hicho kwa kushirikiana na wananchi wake waliomweka madarakani huku jitihada zake ni kuhakikisha anaondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake.

Katika upande wa elimu amesema shule ya msingi Litingi ni miongoni mwa zile zilizozua gumzo nchini kwa kuwa na darasa moja sasa ipo katika mwonekano mzuri baada ya kuboreshwa.


Anasema awali wanafunzi na walimu wa shule hiyo walipata shida kwa kusomea na kuishi katika mazingira duni sasa kwa kushirikiana na wananchi wake wamefanikiwa kujenga madarasa ya kisasa na nyumba za walimu, huku maboresha kuifanya shulle hiyo kuwa ya kisasa yanaendelea.

“Tupo katika hali ya raha, mwazo tulikuwa tukitaabika kwa mvua na baridi, tunamshukuru mbunge wetu Nape Moses Nauye kwa upendo aliotufanyia,” alisema mmoja wa wanafunzi wavulana anayesoma darasa la tatu.


“Siku chache baada ya kuwa mbunge picha ya shule hii ionekana katika mitandao ya kijamii ikisema ni shule iliyo katika jimbo langu, nilichofanya ni kuifuatilia nikaweka kusudio la kuiboresha, na hadi mwaka 2020 itakuwa ni miongoni mwa shule bora,” anasema Nape.

No comments:

Post a Comment