Thursday, 22 March 2018

Nondo asomewa mashtaka ya kudanganya kutekwa


Abdul Nondo 

Regina Mkonde

MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP), Abdul Nondo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa akishtakiwa kwa mashtaka mawili ya kutoa taarifa za uongo mitandaoni na kudanganya kutekwa.

Amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo John Mpitanjia na Wakili wa Serikali, Abel Mwandalama, amekana na kesi yake itatajwa Machi 26, mwaka huu, yupo rumande kwa kunyimwa dhamana.

Wakati huo huo, mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itaanza kusikiliza maombi ya Jinai Na. 49/2018 yaliyofunguliwa mahakamani hapo na watetezi wa haki za binadamu dhidi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Waombaji hao wameitaka mahakama kutoa amri ya Nondo kupewa dhamana. Jaji anayesikiliza maombi hayo,  Rehema Sameji ameitaka Jamhuri kuyajibu hapo Machi 26 na upande wa waleta maombi kuleta maombi yao ya ziada Machi 27 mwaka huu, na kwamba mahakama itasikiliza hoja za pande zote mbili Aprili 4 mwaka huu.

Akizungumza baada ya kuahirishwa maombi hayo, Wakili wa upande wa waleta maombi, Jebra Kambole amesema Aprili 4, 2018 mahakama itasikiliza maombi yao ikiwemo mteja wao, ambaye ni Abdul Nondo kupata dhama, kupata haki ya uwakilishi pamoja na kuangalia kama kushikiliwa kwake na Polisi kulikuwa kwa mujibu wa sheria au laa.

No comments:

Post a Comment