Tuesday, 13 March 2018

Polisi: Nondo alijiteka


Abdul Nondo
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema mwanafunzi Abdul Nondo ambaye alizua gumzo wiki iliyopita baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hakutekwa bali alifanya hivyo kwa sababu anazozijua mwenyewe.
Akizungumza leo Dar es Salaam Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema upelelezi uliofanyika umeonesha kuwa Nondo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake na hakutekwa kama watu walivyokuwa wanadhania.
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kushirikiana na  polisi mkoani Iringa tumefanya uchunguzi na ufuatiliaji na kubaini kuwa mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka mwenyewe au kuamua kutoa taarifa hizo kimsingi zilikuwa na maslahi yake binafsi, pengine alizua hilo kwa kutaka kujipatia umaarufu“amesema Mambosasa na kueleza kilichompeleka Iringa kuwa ni mapenzi.

Upelelezi umeendelea kubaini kuwa mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambaye alikuwa akifanya naye mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa, hii ni baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi na kubaini muda ule aliosema ametekwa  simu yake imeendelea kuonesha mawasiliano kati yake na yule binti aliyekuwa anamfuata,“amesema Mambosasa.
Lazaro Mambosasa

Kwa upande mwingine Kamanda Mambosasa amesema Nondo ataendelea kushikiliwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment