Monday, 12 March 2018

Radi yawaua 16 kanisani


Rais wa Rwanda, Paul Kagame
RADI imewaua takriban watu 16 na kujeruhiwa wengine kadhaa kwenye kanisa moja la Kiadiventista nchini Rwanda juzi Jumamosi.
Wengi wa waathiriwa walifariki papo hapo wakati radi ilipiga kwenye kanisa katika wilaya iliyo Kusini mwa nchi eneo la Nyaruguru, kwa mujibu wa meya wa eneo hilo, Habitegeko Francois.
Watu wawili walifariki kutokana na majeraha na wengine 140 walikimbizwa hospitalini na vituo vya afya.
Radi pia ilimuua mwanafunzi eneo hilo siku ya Ijumaa kwa mujibu wa meya.
Ajali hiyo katika eneo lenye milima karibu na mpaka na Burundi, ilitokea saa za mchana wakati waumini walikuwa bado ndani ya kanisa.
Madaktari wamesema watu wangine watatu wako hali mahututi lakini wanapata nafuu, Francois aliiambia AFP.
Amesema katika kisa cha siku ya Ijumaa, radi ilipiga kundi la wanafunzi 18 eneo hilo na kumuua mmoja.
Watatu kati ya wanafunzi hao wamebaki hospitalini huku wengine wakiruhisiwa kwenda nyumbani.

No comments:

Post a Comment