Friday, 9 March 2018

Rais Magufuli awaonya wanaotaka kuandamana


Dk. John Magufuli

RAIS Dk. John  Magufuli ameonya wananchi na vyama vya siasa nchini kuachana na mpango wa kufanya maandamano ya aina yoyote. Ametoa onyo hilo baada ya siku za hivi karibuni kuzagaa kwenye mitandaa taarifa za kuwepo maandamano makubwa nchi nzima.

Ametoa tamko hilo leo , Machi 9, 2018 wakati akizindua Tawi la CRDB-Bank, Chato mkoani Geita na kuwataka waliojiandaa kutekeleza mpango huo waache mara moja vinginevyo watashughulikiwa.

Dk. Magufuli amesema nchi hii ni ya amani, ndiyo maana uvunjifu wa amani ulipoanza kutokea kule Kibiti serikali iliamua kuufuta mara moja.

“Kuna watu wanadhani tunafanya siasa kila wakati, kama wametumwa na baba zao kuandamana, watawasimulia vizuri," amesema.

Amebainisha kuwa wapo Watanzania wachache ambao hawapendi kuambiwa ukweli, wanapenda kuambiwa maneno matamu yasiyo ya mantiki. 

"Mimi niliomba kura kwa wananchi wangu kwa kusema ukweli, nitaendelea kusisitiza ukweli daima,” amesisitiza.

No comments:

Post a Comment