Sunday, 18 March 2018

Rais pekee wa kike Afrika aendelea kushinikizwa ajiuzulu


Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim.
SHIKIKIZO la kumtaka ajiuzulu Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim ambaye ni pekee mwanamke barani Afrika limeongezeka baada ya kushukiwa kwa kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.
Gurib amekuwa akikanusha madai hayo ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kutoka shirika lisilo la kiserikali ambazo zilinuiwa kusaidia katika ada za wanafumzi kutoka jamii maskini.
Anasemekana alizitumia kwa ajili ya matumizi yake binafsi ya nguo na vitu vingine vya thamani. Lakini siku moja baada ya kukataa wazo la kujiuzulu wakili wake Yusuf Mohamed aliwaambia waandishi wa habari wa nchi hiyo kuwa rais huyo huenda atajiuzulu.
Waziri mkuu wa nchi hiyo amesema rais huyo angeachia wadhifa wake Jumatatu iliyopita, jambo ambalo halikufanikishwa . Gurib amekuwa akisema fedha hizo alizirudisha na hivyo hana kosa lolote.

No comments:

Post a Comment