Wednesday, 14 March 2018

RC Gambo awaonya watakaoandamana

Mrisho Gambo

Mwandishi Wetu, Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa onyo kwa watu watakaothubutu kuandamana mkoani humo.

Ametoa onyo hilo baada ya kuzagaa taarifa mitandaoni kuwa April 26 kutakuwa na maandamano nchi nzima.

RC Gambo amesema Arusha ni jiji la kitalii hivyo asingependa kuona usalama na amani vinatoweka ambavyo vitapelekea kushuka uchumi wake.
Arusha ni mkoa wa kitalii hatuwezi kuruhusu mambo yatakayoharibu uchumi na usalama wetu, kama kuna kikundi kinampango wa kutujaribu, tunatoa tahadhari na kuwakumbusha kuwa upanga haujaribiwi shingoni,amesema.

Kauli ya Gambo ni muendelezo wa maonyo mengine yaliyotolewa na viongozi wengine serikali akiwemo Rais Magufuli kuhusu watu watakaoandamana siku hiyo.    

No comments:

Post a Comment