Sunday, 18 March 2018

RC Makonda awapa shavu wasanii


Paul Makonda


MKUU wa Mkoa (RC) wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaowazuia wasanii kurekodi video za nyimbo au tamthilia kwenye mandhari mbalimbali za jiji kwa kuwa inalorudisha nyuma utalii.

“Haiwezekani msanii akitaka kurekodi video au tamthilia kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa jiji letu hasumbuliwi vibali lakini akirekodi kwenye hotel, majengo marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kibali, hili haliwezekani.

“Kuanzia sasa wasanii mtarekodi video zenu sehemu yoyote mnayotaka isipokuwa ikulu, mahakamani, maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu,” amesema RC Makonda.

Lengo la Makonda ni kuona wasanii wanapewa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia kazi za sanaa wanazofanya.


 RC Paul Makonda (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii hapa nchini.

No comments:

Post a Comment