Mary Meshack,Dodoma
MAHAKAMA ya Rufani ya Tanzania inayoendelea na
vikao vyake kanda ya Dodoma , imesikiliza mashauri 12 tangu ilipoanza Februari
26, mwaka huu.
Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Eddie Fussi
akizungumza leo na wanahabari mjini hapa, amesema mashauri mengine mawili ya
jinai na moja la rufaa ya madai yanatarajiwa kusikilizwa kesho.
Fussi amebainisha mashauri hayo yaliyokwisha sikilizwa
kuwa ni manane ya rufaa za jinai, mawili ya rufaa za madai na mengine mawili ya
rufaa za maombi.
Kwa mujibu wa Fussi mashauri yote
yaliyosikilizwa yamepangiwa tarehe ya kutolewa hukumu na yaliyobaki yanaendelea
kusikilizwa katika vikao hivyo vinavyotarajiwa kutamatishwa mwezi huu (Machi).
No comments:
Post a Comment