Monday, 19 March 2018

Samia afanya ziara visiwa vya PembaSamia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwasili katika uwanja wa ndege visiwani Pemba.


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya siku tatu visiwani Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya jana na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa vyama na serikali, alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba.

Aidha, amewataka wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani. Ametoa kauli hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.
Leo Makamu wa Rais anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika kituo cha huduma za mama na mtoto, eneo la  Shumba Vyamboni.


No comments:

Post a Comment