Sunday, 4 March 2018

Serikali yajipanga kuboresha TGFA


Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo Dar es Salaam. Anayemsikiliza ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Tito Kasambala


SERIKALI imejipanga kuboresha Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), ambayo inasimamia na kuendesha ndege ambazo zinasafirisha viongozi wa kitaifa.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembele na kukagua utekelezaji wa majukumu ya wakala huyo.

Mhandisi Nditiye amesema azma ya Serikali ya Awamo ya Tano ni kuhakikisha taasisi zake zinafanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kufanikisha malengo yake  ya kuwatumikia wananchi.


Naye Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu wa TGFA,  Tito Kasambala amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa taasisi yake ina ndege nne ambazo zinatumika kusafirisha viongozi wa kitaifa katika kutimiza majukumu yao.


No comments:

Post a Comment