Wednesday, 21 March 2018

Serikali yatenga bilioni 5/- kukabili TB


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto akionesha dawa ya kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo jana Dar es Salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.Peter Simon

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga sh.bilioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa mashine za kupima ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), katika zahanati na vituo vya afya nchini. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo wakati akizindua dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 14 hadi 0 jana Dar es Salaam. 

“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga sh.bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi wa haraka ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert” amesema Waziri Ummy. 

Aidha, ametoa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya ugonjwa huo kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure. 

Hali kadhalika amepiga marufuku waganga wa tiba asili kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu, badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka. 

Waziri huyo amesema takribani watu 160,000 nchini wana maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa makadirio ya mwaka juzi (2016).

No comments:

Post a Comment