Friday, 23 March 2018

Tatizo la nguvu za kiume linaweza kumalizwa kwa matunda na mboga za majani


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

UNAWEZA ukawa na afya nzuri katika nyanja nyingine zote lakini ukahujumiwa kifikra kama mahitaji ya mwanaume kuwa lijali siyo kamilifu.

Uwezo wa mwanaume kujamiina na afya kwa ujumla vina uhusiano wa moja kwa moja na lishe bora kinyume cha imani za kutumia dawa zinazoleta suluhisho la muda mfupi huku zikiathiri ubongo na kupoteza fedha.

Sayansi inakubaliana na imani kuwa matunda na mboga vinaongeza nguvu za kiume. Matunda na juisi za mboga vina viini hai vinavyoamsha hamu ya kufanya mapenzi.

Ili kurekebisha au kutibu hali inayosababisha uhanithi, mhusika anapaswa kutumia nafaka, matunda, nyama na mboga za majani.

Ni vema atumie unga wa ngano isiyokobolewa, maharage ya soya, shayiri na karanga. Pia atumie samaki, maini, kuku wa kienyeji na maziwa yaliyoondolewa mafuta, mchicha, juisi ya kabichi, spinachi, kitunguu swaumu, karoti na pilipili hoho.

Anatakiwa pia atumie ndizi, papai, pera, tango, aloevera, afanye mazoezi ya viungo na kuzingatia tiba ya maji, anywe juisi ya mchanganyiko wa karoti na spinachi, ale matango, tofaa na matunda ya mlonge yana madini ya chokaa na sulpher.

Ili kuhakikisha matokeo mazuri, nafaka, matunda, nyama na mboga, viliwe kwa kupokezana katika siku kwa siku na kimoja katika kila fungu.

Katika ili kupata matokeo mazuri ya kutumia tiba tajwa ni vema mwenye tatizo akaja kituoni kwetu ambapo atafafanuliwa namna sahihi ya kutumia tiba tajwa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment