Wednesday, 28 March 2018

Tembo anayetoa 'moshi' mdomoni aonekana India


HUKO India, imeoneshwa video ya tembo anayetoa majivu yanayogeuka kuwamoto hali ambayo imewashangaza wataalamu wengi wa wanyama wa porini duniani.
Vinay Kumar ni mwanasayansi wa hifadhi ya wanyama pori katika jamii ya watu wa India, alipiga picha ya video ya sekunde 48 wakati yuko katika safari ya kikazi katika msitu wa Nagarhole kwenye mji wa Karnataka April mwaka 2016.
Amewaambia BBC kutoionesha video hiyo hadi sasa kwa sababu hakutambua umuhimu wa video hiyo sana.
Wanasayansi wanasema hadi sasa hawaelewi ni kwa nini tembo huyo alikuwa anatoa majivu.
Hifadhi ya wanyamapori nchini India inasema hii ni video ya kwanza inayoonesha makala ya tembo akionesha tabia ya namna hiyo jambo ambalo limewaacha na bumbuwazi wanasayansi pamoja na wataalamu wa wanyama pori.
Kumar amesema yeye na wenzie walitembelea katika msitu huo nyakati za asubuhi ili kuona kama camera zao walizoziweka zimewapiga picha chui. akini wanakuta imempiga picha tembo wa kike aliyekuwa katika umbali wa mita 50 wa kamera.
Tembo huyo alionekana akitoa makaa na kuacha moto chini pindi majivu hayo yanapomtoka.
Kile tulichokiona ni sawa na kuona tembo huyo akivuta alikuwa anatoa majivu mengi kutoka katika mdomo wake na kutoa moshi huo kama alikuwa anavuta.
Mtaalamu wa tembo, Varun Goswami aliichunguza video hiyo na anaamini kuwa inawezekana tembo huyo alikuwa anatoa moto wa makaa, kwa sababu alionekana kama anatoa kitu kutoka chini na kupuliza majivu yaliyokuwa pamoja nayo na kusababisha afanye hivyo.
Aidha, amesema mkaa unajulikana kuwa una athari ingawa unaweza kuwa hauna virutubisho vingi, wanyama pia wanaweza kuvutiwa nao kwa ajili ya tiba.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment