Monday, 19 March 2018

Tigo, Uber waingia makubaliano


Simon Karikari (kushoto), akiwa katika moja ya mikutano yake na wanahabari Dar es Salaam.

Suleiman Kasei

KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania na ile ya Kiteknolojia Uber zimeingia makubaliano ambayo yatasaidia watumiaji wa usafiri Uber kupata usafiri huo bila kuwa na kifurushi cha mtandao maarufu (bado).

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Dar es Salaam baina ya  wakurugenzi wa kampuni hizo mbele ya wanahabari.

Mkurugenzi wa Tigo Tanzania, Simon Karikari amesema kampuni yao ni moja ina nembo kubwa nchini, hivyo ubia walioingia na Uber utazidi kupanua wigo wao kibiashara.

Karikari amesema wateja wa tigo watapata huduma hiyo bila ya kuwa na kifurushi cha mtandao jambo ambalo litaongeza wateja wa usafiri wa Uber.

"Uber  ni kampuni ya Kimataifa hivyo ubia huu ni ishara tosha kuwa Tigo inakubalika na sisi hatutawaangusha kwani tumeshika asilimia kubwa ya soko la biashara ya mawasiliano ya simu nchini," amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa Tigo ina zaidi ya wateja milioni 11.3 hivyo ni matumaini yao kuwa ubia huo na Uber utachochea ongezeko kubwa la wateja kwa muda mfupi na pande zote kunufaika.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo amesema ubia huo ni muhimu kwao na wateja wao kwa kuwa watapatikana bila gharama.

Msemo amesema madereva ni wateja ambao wanatumia mtandao wa Tigo watakuwa wanawasiliana popote bila gharama jambo ambalo awali iilikuwa changamoto.

Amesema usafiri wa Uber umefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 3,000 na kuhudumia watu zaidi ya 200,000 kwa mwezi hivyo ubia huo utaongeza watumiaji.

Meneja huyo amesema mikakati yao ni kuhakikisha kila mkazi wa jiji la Dar es Salaam anaweka kipaumbele katika kutumia Uber kama njia ya usafiri wa haraka kufika anapotaka.

"Tumekuwepo Tanzania takribani miaka miwili sasa kwa mafanikio makubwa lakini hatua ya leo kuingia ubia na Tigo ni hatua kubwa zaidi kibiashara naamini wateja wataongezeka maradufu," amesema.

Msemo amebanisha kuwa ni matarajio ya kampuni yao kuhakikisha wanafika mikoa mingine kwa siku za karibuni ili kusambaza huduma hiyo.

Amesema kwa miaka miwili huduma ya Uber Tanzania imefanikiwa kuhudumia wageni kutoka nchi 70 duniani ambao wa wana App yao.

No comments:

Post a Comment