Rex Tillerson
WAZIRI
wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yupo ziarani katika mataifa matano
ya Afrika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza barani humo.Katika juma moja la ziara
yake atazitembelea Chad, Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Kenya.
Safari hii iliyoelezwa kuwa
ni muhimu kwa Marekani kuchukua nafasi
ya kuwa sehemu ya ukuaji wa maendeleo ya Afrika.
Tillerson atazuru leo
nchini Ethiopia , nchi ya pili yenye idadi kubwa zaidi ya watu Afrika na moja
ya taifa lenye kukua uchumi kwa kasi barani humo.
Hata hivyo, Ethiopia bado
inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa baada ya kujiuzulu kwa ghafla kwa
waziri mkuu wa nchi hiyo na zaidi ya miaka mitatu ya maandamano ya kuipinga
serikali.
Maofisa wa Marekani
wanasema akiwa Ethiopia Tillerson atakutana na kujadiliana mchakato wa
atakayechukua uongozi na kuhusu vurugu zilizojitokeza na vilevile kiongozi huyo
ataongea na viongozi wa umoja wa Afrika ili kuzungumzia kuhusu migogoro iliyopo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia na Sudan Kusini.
Baadaye wiki hii
ataelekea Kenya, Nigeria, Chad na Djibouti ambao Marekani inaona ni washirika wake
wa karibu wa kupambana na ugaidi na kuleta usalama katika upande wa kikanda.
No comments:
Post a Comment