Saturday, 10 March 2018

Tillerson augua Kenya asitisha shughuli alizopanga kufanya leo


Rex Tillerson
WAZIRI wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya le baada ya hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.
Hakuna ishara yoyote inayoainisha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 anasumbuliwa na tatizo kubwa la kiafya.
Msemaji wake amesema,Tillerson amekuwa kwenye ratiba ngumu katika ziara yake ya Afrika wakati huo huo akitumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya simu kufuatilia kazi nyingine nchini mwake kama vile suala la Korea Kaskazini.
Maofisa wamesema watahairisha baadhi ya ratiba ambazo Tillerson alikuwa ameweka ikiwa ni pamoja na safari yake ya kwenda kuona eneo ambalo ubalozi wa Marekani ulikuwa umelipuliwa mwaka 1998.
Tillerson amekuwa katika ziara ya mataifa matano ya Afrika tangu siku ya Jumatano wiki hii akiwa ameanzia Ethiopia na sasa yuko Kenya kwa siku ya pili.


No comments:

Post a Comment