Tuesday, 20 March 2018

TPDC: Wapuuzeni wanaosambaza taarifa za uongo kuhusu DangoteShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewataka wananchi kupuuza taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba, kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara kimefungwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, kushindwa kwa makubaliano ya mauzo ya gesi asilia baina ya Dangote na TPDC. 

TPDC inawataarifu wananchi kwamba, imetimiza makubaliano yote ikiwemo mauzo ya gesi asilia pamoja na ujenzi wa mitambo ya kusafirishia gesi asilia hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya kiwanda cha Dangote, tangu 2017. 

Aidha, taarifa inayosambazwa katika mitando ya kijamii ya mwaka 2016 imepitwa na wakati. Hivi sasa kiwanda cha saruji cha Dangote kinaendela na mchakato wa usimikaji wa mitambo yake ya kuzalisha umeme wa gesi asilia. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi ujao (Aprili 2018).


No comments:

Post a Comment