Saturday, 10 March 2018

Trump hakupata ushauri wa utawala kukubali kukutana na Kim Jong-un


Rais wa Marekani, Donald Trump (kushoto) na wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
RAIS Trump ameandia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twittter kuwa makubaliano na Korea Kaskazini yapo kwenye mchakato wa kutekelezeka.
Ametoa taarifa hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kukubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Ingawa hadi sasa Korea Kaskazini haijatoa tamko lolote.
Aidha, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence amesema uamuzi wa Korea Kaskazini kutaka kukutana na rais wa Marekani Donald Trump unathibitisha kuwa mpango wa kuitenga Korea Kaskazini unafanya kazi.
Hata hivyo, makubaliano ya mkutano huo wa kihistoria umewashangaza waangalizi licha ya baadaye ikulu ya White House ya Marekani imesema mkutano huo hauwezi kufanyika hadi Korea Kaskazini ichukue hatua thabiti kabla.
Mwezi mmoja uliopita, Rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikuwa wana malumbano makali, lakini sasa Trump amekubali kuhudhuria mkutano huo alioalikwa licha ya kuwa mwaliko huo uliletwa na Korea Kusini.
Vyombo vya habari vya Marekani vimesema Rais Trump alifanya uamuzi wa kukubali kuhudhuria mkutano huo bila kupata ushauri kutoka katika utawala wake.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza barani Afrika amethibitisha kuwa uamuzi huo ni wa Trump pekee na kwamba yeye hakufahamu lolote licha ya kuwa walikuwa na mazungumzo kabla ya tangazo hilo kutolewa.
Ingawa ujumbe huo wa kukaribishwa kwa Trump umekuwa unajichanganya kwa kuwa katibu wake Trump Sarah Sander aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini imeahidi kusitisha mpango wake wa nuklia na wamekubali kufanya hivyo kabla ya mkutano huo.
Trump atakuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini kama mkutano huo utaafikiwa kwa kuwa hakuna kiongozi wa Marekani aliyewahi kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini .


No comments:

Post a Comment