Sunday, 11 March 2018

Trump: Mazungumzo na Korea Kaskazini yatakuwa makubwa kwa dunia


Donald Trump
RAIS wa Marekani Donald Trump amesema mkutano ulipangwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un unaweza kufeli au ulete makubaliano makubwa zaidi kwa dunia.
Wakati wa mkutano wa kisiasa huko, Pennsylvania, Trump amewaambia wafuasi wake kuwa ana amini Korea Kaskazini inataka kuwe na amani.
Lakini amesema ataacha mazungumzo hayo kwa haraka ikiwa hayataangazia suala la kuharibu silaha za nyuklia.
Katika hotuba yake, Trump ameonya kuhusu kodi kwa magari ya Ulaya na kuzindua kauli mbiu yake ya kuchaguliwa tena mwaka 2020.
Amesema ana matumaini kuwa makubaliano ya kupunguza misukosuko ya nyuklia yatafanyika kusaidia nchi kama Korea Kaskazini.
Pia amesema ana amini Korea Kaskazini wataheshimu ahadi za kutofanya majaribio zaidi ya makombora.
Hakuna rais wa Marekani ambaye alishawahi kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini lakini kumekuwa na majaribo kadha ya kuitaka Korea Kaskazini kuachana na mpango wa silaha za nyuklia.
Jitihada kubwa zaidi za mazungumzo ya pande sita yaliyovunjika mwaka 2008, kwa sababu Korea Kaskazini ilikataa kuruhusu wachunguzi kubaini ikiwa Korea Kaskazini ilikuwa imesitisha mipango yake ya nyuklia.
Majaribio kadhaa ya kufufua mazungumzo hayo yalishindikana, ikiwemo mwaka 2012 wakati Korea Kaskazini ilirusha kombora lingine, wiki mbili baada ya kutangaza makubaliano na Marekani.

Kim Jong-un yuko chini ya vikwazo kadhaa vya usafiri. kwa hiyo kuna uwezekano kuwa anaweza kukutana na Trump nchini Korea Kaskazini. Watakutana eneo lenye ulinzi mkali kwenye mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini au labda huenda mkutano wao ukafanyika China.

No comments:

Post a Comment