Friday, 30 March 2018

Tule vyakula mchanganyiko kuepuka maradhiMtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

KIMSINGI kuna aina nne za makundi ya vyakula vyetu tunavyokula kila siku. Vyakula hivi ndivyo vinasaidia kujenga miili yetu, kuitia nguvu, kuipa joto na kuilinda.

Tunashauriwa vyakula vyetu tunavyokula kila siku ni vema viwe mchanganyiko unaotokana na makundi manne ya vyakula ili kuuepuka miili yetu kupata maradhi ambayo mara nyingi yanayosababishwa na kukosa moja ya aina za vyakula hivi.

Makundi hayo manne ni vyakula vya kujenga mwili miongoni mwavyo yakiwemo maziwa, kunde, dengu, maharagwe na mayai.

Kundi la pili ni vyakula vya kuutia nguvu mwili ambapo ni pamoja na mahindi, ngano, mtama, mihogo na ulezi.

Kundi la tatu ni vyakula vya kulinda mwili ambavyo ni mboga za majani, matunda na aina zote za vyakula vyenye vitamin.

Kundi la nne ni la vyakula vya kutia joto mwili ambavyo ni pamoja na karanga, korosho, ufuta, mbegu za maboga, alizeti, mahindi na mafuta.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment