Monday, 12 March 2018

Tumia hivi kuondoa upele

UPELE ni ugonjwa wa ngozi ambao unasababishwa na ukosefu wa viini vya kutosha katika chakula pamoja na uchafu wa mwili na mazingira yake. Mgonjwa wa upele anajisikia kuwashwa na hivyo kujikuna wakati wote.

Upele unaweza kuwa mdogo kama wa surua au mkubwa kama wa tetekuwanga. Zipo tiba mbalimbali zinazoweza kusaidia tatizo hilo miongoni mwazo ni bizari, karela, ndimu, mnanaa, ndizi na muarobaini.

Bizari

Ponda vikonyo viwili au vitatu vya bizari ongeza na maji ya kutosha kupata urojorojo, baada ya kuoga paka sehemu zilizoathirika na tatizo hilo wakati wa asubuhi na jioni.

Pia tengeneza glasi moja ya bizari na ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asali. Kunywa, endelea na tiba hii kwa muda wa siku 10 utaona mabadiliko makubwa ya tatizo lako.

Karela na ndimu

Andaa juisi ya matunda mawili ya karela, kamulia ndimu kisha kunywa wakati wa asubuhi kabla ya chakula chochote na jioni kabla ya chakula cha usiku. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku nne.

Mnanaa

Chukua mnanaa uponde , ongeza maji ya kutosha, paka sehemu za mwili zilizoathirika kwa upele. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku 10.

Ndizi na muarobaini

Chukua ndizi iliyowiva vizuri yenye rangi ya njano, changanya na maji ya muarobaini yaliyopatikana baada ya kuyachemsha, paka mwili mzima, baada ya saa moja oga. Endelea na tiba hii kila asubuhi na jioni kwa muda wa siku 10.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia virutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment