Friday, 2 March 2018

Tumia kitunguu swaumu na ndimu kuondoa chawa
CHAWA ni miongoni mwa wadudu wadogo wanaoendeleza uhai wao kwa kunyonya damu za viumbe wengine akiwemo binadamu.

Wadudu hao wanaotisha unapowaona, wanaweza kuishi kichwani au katika nguo za binadamu ili kupata fursa ya kumnyonya kwa urahisi.

Mtu au mnyama mwenye chawa huwa anajikuna mara kwa mara. Licha ya binadamu chawa pia wanaishi katika miili ya wanyama wengine akiwemo nguruwe.

Kimsingi tatizo la chawa kichwani husababishwa na uchafu hususan kwa wasioosha kichwa mara kwa mara hasa baada ya kufanya kazi nzito za kutoka jasho jingi.

Mtu pia anaweza kupata chawa kwa kuambukizwa baada ya kushirikiana vifaa vya kutengenezea nywele na mtu mwenye wadudu hao au hata kulala pamoja na mwenye chawa.

Ili kuondokana na wadudu hao wanyonyaji, unaweza kutumia kitunguu swaumu na ndimu.

Changanya kitunguu swaumu kilichopondwa pondwa pamoja na maji ya ndimu, lowanisha nywele zako vizuri na mchanganyiko huu, baada ya saa mbili osha nywele zako. Rudia tiba kwa muda wa siku mbili. Baada ya kuondokana na chawa hakikisha udumu katika hali ya usafi wa mwili na mavazi.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment