Saturday, 17 March 2018

Tumia moja ya hivi kukabili tatizo la kuchelewa kuzaaMtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akifafanua namna sahihi ya kutumia tiba hizo.


TATIZO la kuchelewa uchungu wa kuzaa limekuwa likiwakumba baadhi ya wajawazito katika maeneo mbalimbali na kwingineko duniani.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa kutumia mimea tiba na matunda yanayostawishwa katika bustani zetu.

Kiazi kikuu, papai bichi na mti wa pamba ni miongoni mwa tiba zinazowasaidia wajawazito wengi kuondokana na tatizo hilo.

Kiazi kikuu

Kula muhogo wa mmea huu mara kwa mara, una uwezo mkubwa wa kulegeza misuli iliyokaza na kuondoa mishtuko, kifafa cha mimba na kusaidia ini. Unazuia pia kuzaa kabla ya wakati kwa kuwa unaweka sawa kizazi.

Papai bichi

Lina tabia ya kuuharakisha uchungu na kufikia hatua ya kujifungua haraka. Menya papai likate robo kilo na kulichemsha kwa muda wa roba saa, kisha kula lote na kunywa maji yake, fanya hivyo mara mbili kwa siku hadi utakapojifungua.

Nanasi

Chukua pia majani ya nanasi nusu kilo, ponda na kutengeneza juisi lita moja na nusu kunywa glasi moja mara mbili kwa siku hadi siku utakapojifungua.

Mti wa pamba

Nusu kilo ya maganda ya mti wa pamba yaponde, yachemshe kwa muda wa dakika 15 katika lita moja na nusu ya maji, baada ya kupoa kunywa glasi moja mara mbili kwa siku hadi wakati wa kujingua.


Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho, anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment