Saturday, 24 March 2018

Tumia moja ya tiba hizi kuimarisha machoMACHO ni miongoni mwa viungo muhimu kwa binadamu ambavyo vinamwangazia popote anapopita au sehemu anayotekeleza majukumu yake ya msingi yanayompa riziki yake ya kila siku.

Na ikitokea jicho au macho yakapatwa na tatizo hususan la uoni hafifu au kutokuona kabisa au maumivu inamfanya mwanadamu awe katika wakati mgumu kwa kuwa pamoja na mambo mengine mwili wake huingiwa kiza.

Zipo tiba nyingi asilia ambazo zinasaidia tatizo hilo, ikiwemo mlonge, bizari, tetere na uwatu.

Bizari

Tumia kijiko kimoja kutwa mara tatu katika maziwa freshi au maji moto

Uwatu

Tumia kijiko kimoja kutwa mara tatu katika maziwa freshi au maji moto.

Mlonge

Kijiko kimoja kutwa mara tatu katika maji moto ongeza na asali kidogo, kunywa kisha tenga nyingine kidogo ili kunawa uso au kuipaka usoni  hususan ile iliyochunjwa.

Tetere

Twanga na kuzinywa katika glasi au tafuna mbegu za maboga kila siku muda wa mwezi na zaidi.

Jambo la kuzingatia ni kwamba iwapo umekumbwa na tatizo hilo fika katika ofisi zetu ambapo utapata maelezo ya kina ya namna ya kutumia kila moja ya tiba hiyo kutoka kwa mtaalamu wetu. 

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment