Wednesday, 28 March 2018

Tumia moja ya tiba hizi kumaliza tatizo la chunusiKUTOKWA vipele usoni  (chunusi), ni tatizo linalohitaji tiba, isiyo na madhara licha ya kuwa baadhi ya wanawake wanapaka krim kali ambazo wakati mwingine zinawachubua ngozi.

Tatizo hili kitaalam linasababishwa na nywele ndani ya ngozi ya kichwa kutoa mafuta ya kulainisha ngozi. Safari ya mafuta hayo huwa mengine yanakwama katika njia na kufanya bakteria kuzaliana na kuzalisha maumivu na viuvimbe.

Zipo tiba mbalimbali za asili zisizo na madhara zinazoweza kumaliza tatizo hilo miongoni mwazo ni tango, papai, aloevera na kitunguu swaumu.Tango

Tengeneza juisi ya tango na kunawia uso asubuhi na jioni kwa muda wa juma moja au kata kipande cha tango paka utomvu wake usoni acha kwa muda wa robo saa kisha nawa.

Limau

Tumia juisi ya limau kupaka usoni kila usiku unapokwenda kulala na kunawa asubuhi. Pia pendelea kutumia juisi za matunda kila siku.

Papai

Vijiko vitatu vya juisi ya papai changanya na ya limau kijiko kimoja paka usoni mchanganyiko huo kila baada ya kunawa. Iache usoni kwa muda wa nusu saa kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.

Kitunguu swaumu

Punje tano za kitunguu swaumu kilichopondwa tia katika glasi yenye maji moto, kunywa mara moja kwa siku au chemsha punje 20 zilizopondwa katika maji ya glasi moja kisha kunywa kijiko kikubwa 1,kutwa mara 4.

Hata hivyo, ni vema unapokumbwa na tatizo hilo uje makao makuu ambapo unaweza kupata maelezo ya kina ya namna ya kutumia tiba hiyo kutoka kwa mtaalam wetu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment