Friday, 23 March 2018

Tumia tangawizi na ufuta unaposhikwa na maumivu ya hedhi

NI jambo la kawaida wakati wa hedhi kusikia maumivu kidogo, kukosa raha, kubana misuli ya miguu na mapaja.

Ni dalili za kawaida. Wakati mwingine hali inakuwa mbaya zaidi ambapo mhusika anapata maumivu makali ya mgongo, tumbo na hata kutokwa damu nyingi.

Msongo wa kisaikoloji na wasiwasi huwa vinatangulia kabla ya kubana misuli, maumivu makali na kuanza kutoka damu kidogokidogo vinafuata.

Mgonjwa anapokuwa na hali ya uoga huathiri misuli kufanya kazi yake vilivyo, hivyo kusababisha kuganda kwa damu na kupelekea maumivu zaidi.

Maumivu yanapozidi wakati mwingine mgonjwa atapata kiherehere cha moyo pamoja na kizunguzungu. Unaweza kuondokana na tatizo hili kwa kutumia tangawizi na ufuta.

Tangawizi

Ziponde tangawizi mbichi, chemsha ndani ya maji ya kutosha kwa dakika 10, ongeza sukari kidogo halafu chuja. Kunywa glasi moja ya maji hayo kutwa mara tatu, fanya hivyo baada ya kula. Matibabu haya unaweza kufanya siku tatu kabla ya kuingia katika hedhi na wakati wa hedhi.

Ufuta

Saga glasi moja ya ufuta, siku tatu kabla hujaingia katika hedhi kunywa glasi moja ya maji moto uliyochanganya na nusu kijiko cha chai cha unga wa ufuta. Fanya tiba mara mbili kwa siku  hadi kipindi cha hedhi kinapomalizika.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment