Sunday, 4 March 2018

Tumia utomvi wa papai kutibu kidonda nduguMtaalam Abdallah Mandai

KIDONDA ni jeraha linalojitokeza katika mwili wa binadamu kutokana na sababu mbalimbali iwe kukatwa au kuchomwa na kitu chenye ncha kali au uvimbe unaosababishwa na jipu.

Muda wa tiba ya kidonda unategemea ukubwa wake, chanzo, dawa za awali ambazo zimetumiwa kutibu, kama ni cha muda mrefu ni vema mgonjwa awasiliane na mtaalamu wa tiba asili kwa maelezo ya ziada ili kufanikisha tiba yake.

Miongoni mwa tiba ambazo unaweza kutibu kidonda ni utomvu wa papai asali, zabibu, mianzi, kitunguu maji, mtunguja na tambuu.

Utomvu wa papai

Changanya utomvu wa papai na matuta ya ng’ombe, paka kwenye kidonda asubuhi na jioni. Tiba hii inasaidia hata kwa wenye vidonda ndugu.

Asali

Safisha kidonda kwa maji safi yaliyochemshwa na kuongezwa chumvi ya kutosha. Paka asali kwenye kidonda asubuhi na jioni.

Zabibu

Chukua zabibu zilizokaushwa, pondaponda ili kutengeneza aina ya ujiuji, chukua kitambaa safi kinachotosha kuenea sehemu yote yakidonda, paka ujiuji wa zabibu kwenye kitambaa hicho, kiweke kingine kinacholingana juu yake, bandika kwenye kidonda funga na kingine.

Zabibu ina uwezo wa kunyonya sumu kutoka kwenye kidonda. Rudia utaratibu huo mara nne kwa siku.

Mianzi

Kata chipukizi la mianzi, ponda na ulitumie kuoshea kidonda kila asubuhi. Chukua gramu 100 za majani ya mianzi, chemsha katika milimita 300 za maji hadi yabaki milimita 200, asubuhi kunywa milimita 100 na kiasi hicho inayobaki itumie jioni.

Kitunguu maji

Ponda kitunguu maji, kisha maji yake yapake kwenye kidonda kilichosafishwa, fanya hivyo asubuhi na jioni hadi kidonda kitakapo pona.

Mtunguja

Chukua majani ya mtunguja, osha vizuri ndani ya maji moto , ponda halafu bandika kwenye kidonda kilichosafishwa kwa maji ya chumvi au muarobaini. Fanya hivyo asubuhi na jioni kama kidonda bado hakijakauka.

Mtunguja ni dawa nzuri kwa vidonda vikubwa na pia vidogo ambavyo vimedumu kwa muda mrefu bila kupona.

Tambuu

Ponda majani ya tambuu, kamulia maji yake kwenye kidonda kilichosafishwa vizuri. Bandika jani la tambuu kwenye kidonda kama bandeji.

Endelea na matibabu hayo kwa muda wa siku tatu hadi saba kwa kutegemea ukubwa wa kidonda.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo au ushauri wa kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment