Sunday, 4 March 2018

Uamuzi wa SPD kuhusu Serikali ya mseto Ujerumani unasubiriwa


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel 

UJERUMANI inasubiri kwa hamu matokeo ya uamuzi wa chama cha Social Democrats (SPD), kuhusu iwapo wanachama wake wataridhia chama hicho kijiunge kwa mara nyingine tena katika serikali ya mseto na chama cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel cha Christian Democratic Union CDU na chama ndugu cha Christian Social Union CSU.

Kura ya hapana kutoka kwa SPD, miezi mitano tangu uchaguzi mkuu wa Septemba 24, huenda ukalitumbukiza taifa la Ujerumani ambalo ndilo imara zaidi kiuchumi barani Ulaya katika mzozo zaidi wa kisiasa.

SPD inatarajiwa kutangaza uamuzi uliofikiwa na wanachama wake zaidi ya 460,000 mwendo kwenye makao makuu ya chama hicho yaliko mjini Berlin.

Iwapo CDU/CSU na SPD vitashindwa kuunda serikali, basi Merkel huenda akalazimika kuongoza serikali iliyo ya wachache au uchaguzi mpya kuitishwa.

Chanzo: DW

No comments:

Post a Comment