Friday, 9 March 2018

Ucha-Mungu wa viongozi unaondoa ubinafsi- Pinda
Mizengo Pinda

Mary Meshack, Dodoma

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amewataka viongozi kuwa waadilifu na wachamungu kwa kuwa tabia hiyo itawafanya waache kufanya kazi kwa ubinafsi, chuki na kula rushwa.

Pinda ametoa kauli hiyo alipokuwa akifunga kongamano la maombi ya kuliombea taifa pamoja na viongozi, ambalo limeratibiwa na Kingdom Leadeship Netwark Tanzania.

Amesema ili uweze kuwa na taifa lenye viongozi waadilifu ni lazima jamii nzima imche Mungu ndipo miongoni mwao wanaweza kupatikana viongozi hao.

Amefafanua kuwa viongozi wote ndani ya serikali, kwenye vyama vya siasa pamoja na taasisi mbalimbali ni lazima wafanye kazi kwa hofu ya Mungu kutoka moyoni na siyo kwa kuzingatia maigiizo.
"
Maombi ambayo yamekuwa yakifanyika kwa ajili ya kuliombea taifa pamoja na viongozi mbalimbali, yawe chachu ya kuwaletea maendeleo wananchi na viongozi wanatakiwa kuitambua wazi kuwa ili nchi iweze kuwa na maendeleo ni lazima kuwepo na utawala bora,” amesema.

Licha ya hayo, Pinda pia amesema kuna haja ya kuanzishwa vikundi vya maombi kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuwekeza njia bora ambayo watoto watakiwa waaminifu katika utendaji wao.

Kwa upande wake kiongozi aliyekuwa makamu wa benki ya dunia kanda ya Afrika, Dk. Oby Ezekwesili kutoka nchini Nigeria akitoa mada katika kongamano la maombi kuhusu utawala bora, uwazi na uwajibikaji amesema ili nchi iweze kusonga mbele ni lazima kuwa na viongozi wanazingatia misingi ya utawala bora.

No comments:

Post a Comment