Tuesday, 6 March 2018

Ugonjwa wa Listeria nyama kutoka Afrika Kusini yasusiwa


Bidhaa za nyama ya kushindikwa zimeondolewa sokoni
SERIKALI ya Afrika Kusini imezitaja nyama za kusindika aina ya Polony kuwa na sumu iliyosababisha vifo vya watu 180. Na imewashauri watu kutotumia nyama yoyote ya kiwandani.
Amri hiyo imetolewa kwa wenye maduka kurudisha bidhaa hizo na kuziondoa kabisa katika maduka yao.
Nchi zilizozuia uingizaji wa nyama hizo kutoka nchini Afrika Kusini ni pamoja na Namibia, Msumbiji, Malawi, Botswana na Zambia.
Waziri wa kilimo na usalama wa chakula wa Msumbiji amekaririwa kuwa wamiliki wote wa maduka yanayouza nyama hizo waanze kuziondoa mara moja kwenye maduka yao kutokana na hatari inayodhuru afya.
Imechukua zaidi ya mwaka mmoja kwa nchi ya Afrika Kusini kugundua tatizo hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kumekuwa na kesi 948 za sumu ya Listeria nchini Afrika Kusini ambapo Umoja wa Mataifa umeziita ni shambulizi kubwa kuwahi kutokea
Chanzo cha ugonjwa huo wenye sumu inaaminika kuwa umetoka katika kiwanda kilichopo Kaskazini mwa jiji la Polokwane, ambao unatengeneza vyakula vya aina mbalimbali.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Tiger, ambayo inamiliki viwanda hivyo anasisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote’ kati ya bidhaa anazozalisha na watu 180 waliokufa.
Kwa upande wake, Lawrence McDougall amesema kampuni yake walikuwa wametoa tahadhari ya kutazamwa upya kwa tangazo hilo la serikali.
Kampuni mwenza ya vyakula inayojulikana RCL nayo imekumbwa na tuhuma hizo hali iliyopelekea kusimamisha uzalishaji wa nyama.
Baada ya Mamlaka za Afya kuagiza kusitishwa kwa nyama hizo, maduka makubwa (supermarkets) ikiwemo Shoprite, Pick n Pay, Spar na Woolworths tayari zimeshaondoa bidhaa hizo, za bacon na nyingine za nyama ya kusindikwa.
Baadhi ya wateja waliamua kurudisha bidhaa ambazo walikuwa wamenunua na kutaka kurudishiwa gharama zao.
Ofisa mmoja wa taasisi ya taifa ya magonjwa ya mlipuko ameliambia gazeti la Times libe kuwa kumekuwepo na uhaba wa vipimo vinavyotumika kuangalia bakteria aina ya Listeria kwa muda wa wiki mbili katika kiwanda cha Polokwame
“Bakteria wa Listeria ni vigumu kugundulika kutokana na kujificha kwenye nyufa za viwanda,”anasema.
Wateja waliokuwa wametunza bidhaa hizo aina ya Colony kwenye majokofu wameshauriwa kuziteketeza .
Inaweza kupatikana kwenye vyakula vilivyobeba bakteria aina ya listeria au kuwa karibu katika mashamba ya wanyama pia inaweza kupatikana kwenye chakula ambacho hakijapakiwa ikiwa ni pamoja na sandwich na pate.
Dalili zake ni pamoja na kuwa na joto kali, mafua, kuhara na kutapika, watu walioathirika wanaweza wasioneshe dalili zozote, lakini kwa wazee na vijana wanakuwa katika mazingira magumu zaidi.

No comments:

Post a Comment