Monday, 19 March 2018

Ukipatwa tatizo la kufunga choo zingatia haya


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akielezea namna ya kukabiliana na tatizo la kufunga choo huku akiwa ameshika moja ya virutubisho vinavyosaidia kukabiliana na maradhi mbalimbali.

KUFUNGA choo ni hatua ya utumbo mkubwa kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kwa kuwa ndiyo mkondo wa mwisho wa kupitisha chakula.

Dalili za tatizo hilo ni kutokwenda chooni kwa siku nzima au zaidi, kinyesi hugeuka na kuwa kigumu zaidi wakati wa kuchutama, utando mweupe kwenye ulimi, chunusi kwa wingi ambazo hutokana na hamu ya kula kutoweka na maumivi ya kichwa, mgongo, kiungulia, kukosa usingizi na kizunguzungu.

Kinga

Usipende kula vyakula vilivyokobolewa, usivimbiwe, kila siku unywe maji ya kutosha, usile nyama kupita kiasi, epuka vyakula vya ngano mpya. Tumia mikate ya muda walau iliyookwa baada ya saa 24 zilizopia.

Pia ni vema ukawa na muda maalum wa kula badala ya kutafuna kila wakati, pia fanya mazoezi na kutumia dawa kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam tiba.

Tiba zake

Nenda chooni kachutame hata kama hujusikiii kwenda haja, kula kwa wingi vyakula vya kijani, majani na matunda yaliyowiva, kula kikombe kimoja cha majani ya mlonge yaliyopikwa pamoja na mlo na unaweza kula kipande kikubwa cha papai lililoiva kama kinywaji kabla ya mlo wa asubuhi.

Kula mapera matatu makubwa yaliyowiva kwa muda wa siku tano hadi saba, lazima choo kitafunguka.

Tumia juisi ya aloe vera kwa muda wa siku tano pia loweka usiku kucha ndani ya glasi maganda ya malimau mbili zilizokatwa pamoja na mbegu zake, chuja na tumia kabla ya kula.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment