Monday, 26 March 2018

Unajua mbegu ya dodoki kiboko ya maradhi ya kuhara damu?UCHUNGUZI wa kitaalamu unasema kuhara damu kunasababishwa na vijidudu wanaozaliana katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa.

Vijidudu hao wapo wa aina mbili, protozoa ambao husababisha amiba na basillari ambao husabisha kuhara damu.

Kinachohamasisha uzalishaji wa vijidudu hao ni kuoza kwa protini ya ziada inayotokana na vyakula aina ya nyama, vya mafuta ambavyo siyo rahisi kuyeyushwa ndani ya tumbo, vyakula vya kukaangwa, vyakula vyenye viungo vingi, ulaji ovyo ovyo, watu kusongamana katika mazingira machafu au  matatizo  ndani ya tumbo.

Mgonjwa wa kuhara damu anajisikia kwenda haja kubwa mara kwa mara na awapo chooni anajikuta anatoa kinyesi kidogo chenye damu na utando kama kamasi huku akishikwa na maumivu makali ya tumbo au homa.

Ni vema mgonjwa wa kuhara damu akapatiwa matibabu ya haraka, huku akila matunda na mboga za majani kwa wingi, chakula kisicho na mafuta mengi na cha nafaka.

Licha ya tiba za kisasa unaweza kutibu tatizo la kuhara damu kwa mbegu za dodoki, banyani, mbegu za hina, mkaa au jivu, kitunguu swaumu, limau, ndizi, ufuta na samli.

Mbegu za dodoki

Saga mbegu za dodoki zilizokauka ili kupata unga laini, tumia kijiko kimoja cha chai cha unga huo katika maziwa glasi moja mara tatu kwa siku muda wa  siku saba. Tumia maziwa kama chakula  wakati wote wa tiba hadi tatizo litakapokuwa limekwisha.

Tiba hii inafaa zaidi kwa mgonjwa anayeharisha damu inayosababishwa na amiba.

Banyani

Majani ya banyani yaloweke kwa muda wa saa 12 kunywa maji hayo mara tatu kwa muda wa siku saba.

Mbegu za hina

Tengeneza unga kwa kutumia mbegu za hina, changanya nusu kijiko cha chai cha unga wa hina na samli kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Mkaa au jivu

Kijiko kimoja cha unga wa mkaa changanya katika glasi moja ya maji moto, kologa kunywa baada ya kuwa vuguvugu, fanya hivyo mara tatu kutwa kwa muda wa siku tatu.

Kitunguu swaumu

Kula punje tisa za kitunguu swaumu kila siku kwa muda wa siku saba, iwapo utaona vigumu kutafuna, ponda halafu kula pamoja na maziwa au maji.

Limau

Menya limau nne zikate katika vipande vidogo, vitie katika nusu lita ya maji, chemsha jikoni kwa muda wa dakika tano, kisha chuja kunywa juisi hiyo kutwa mara tatu. Tumia tiba hii kwa muda wa siku saba.

Ndizi za kupikwa

Pika ndizi zinazofaa kwa mlo wa mtu mmoja, ziponde hadi ziwe laini sana, ongeza chumvi kidogo, tumia chakula hii kama mlo pekee wakati wote. Tiba hii ni kwa mgonjwa wa kuhara damu.

Ufuta na samli

Saga ufuta vijiko viwili vya ufuta uliokaangwa ili kupata unga laini. Changanya kijiko kimoja cha mezani cha unga huo katika samli. 

Mchanganyiko huo uweke katika nusu lita ya maziwa ya mbuzi, chemsha kwa muda wa dakika tano, kunywa robo glasi mara tatu kwa siku muda wa siku saba.

Hata hivyo, ni vema kabla ya kutumia tiba husika uje makao yetu makuu ambapo mtaalam wetu atakupa maelezo stahiki ya namna ya bora ya kutumia mbegu ya dodoki na tiba nyingine tajwa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment