Thursday, 15 March 2018

Unapoumia usijikande tumia moja ya tiba hiziMtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akifafanua namna sahihi ya kufanya baada ya kuumia.

INASHAURIWA unapoumia na uvimbe kujitokeza si vema kukanda kwa kuwa kunaweza kuongeza uvujaji wa damu ndani kwa ndani hivyo kukuongezea uvimbe

Badala yake ni vema ukatumia tiba zifuatazo kukabiliana na tatizo hilo ambazo ni pamoja na bizari, chokaa, asali, ukwaju, chumvi, kitunguu swaumu, mafuta ya mkaratusi na ya taa.
Bizari na chokaa

Changanya bizari na chokaa, ongeza maji kidogo koroga ili vichanganyike ipasavyo kisha ubandike sehemu yenye maumivu kwa muda wa saa moja kutwa mara tatu.

Chokaa na asali

Asali na chokaa vichanganye vizuri kisha bandika katika uvimbe kwa muda wa saa moja, mara tatu kwa siku.

Ukwaju na chumvi

Juisi nzito ya ukwaju changanya, ongeza chumvi nyingi, koroga vizuri, paka uji huo sehemu zote zenye uvimbe unaotokana na kuumia au kuteguka, uache kwa muda wa saa 12 kisha paka mwingine, endelea hivyo hadi utakapopata nafuu.

Chokaa, kitunguu swaumu na bizari

Mchanganyiko  wa vitu vyote vitatu paka sehemu uliyoumia na kuteguka, acha mchanganyiko huo ukaukie sehemu ya tiba kwa muda wa saa 12, osha na rudia tena, endelea hivyo hivyo hadi nafuu itakapopatikana.

Mafuta ya mikaratusi, taa

Chovya kitambaa laini au pamba ndani ya mafuta ya mkaratusi au ya taa. Kanda taratibu sehemu yenye uvimbe au maumivu yaliyosababishwa na mshtuko. Tumia tiba hii mara tatu kwa siku.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment