Friday, 30 March 2018

Upelelezi kumbainia askari aliyemwua Akwilina unaendelea - MambosasaLazaro Mambosasa 

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema uchunguzi dhidi askari polisi wanaotuhumiwa kwa kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwina Akwiline bado unaendelea na haijajulikana ni silaha ipi iliyotumika.

Akizungumza na wanahabari leo Dar es Salaam, Kamanda Mambosasa amesema kama walivyotoa taarifa kutuhumiwa kwao na hata upelelezi utakapo kamilika wataeleza.

“Askari waliokuwa wametuhumiwa kuhusu kifo cha Akwilina ikumbukwe kwamba walivyokamatwa tulieleze bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile," amesema.

Kwahiyo bado suala la upepelezi unaendelea yapo maelekezo ambayo yaliyotolewa. Ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndiyo iliyokwenda ikamgusa Akwilina lakini askari wale kama mnavyojua walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi ni yupi alikuwa ametenda kwahiyo upepelezi bado unaendelea,“ ameongeza Mambosasa.

Akwilina Akwelina aliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi siku ya Ijumaa Februari 16, 2018 wakati wa maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  wakishinikiza mkurugenzi wa uchaguzi Kinondoni kutoa viapo kwa mawakala wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment