Thursday, 15 March 2018

Upigaji marufuku wa Adhana wazua hisia kali Kigali RwandaMsikiti za zamani ulioko nchini Uingereza
MARUFUKU ya matumizi ya Adhana { Wito kwa Waislamu kuhudhuria swala} katika tarafa ya Nyarugenge, kwenye Jiji la Kigali nchini Rwanda imepingwa vikali na baadhi ya Waislamu jijini humo.
Utawala katika kunakopatikana jamii kubwa ya Waislam nchini humo umebainisha kuwa kumekuwepo muafaka wa kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa kuwasumbua wananchi.
Kulingana na mwandishi wa BBC John Gakuba wito huo wa Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa wananchi.
Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.
Wito huo wa maombi miongoni mwa jamii za Waislamu kote duniani hutumia vipaza sauti na hufanyika mara tano kwa siku.
Licha ya utawala wa eneo hilo kudai kwamba kumekuwa na mwafaka kutoka pande zote mbili baadhi ya Waislamu waliohojiwa wametoa hisia tofauti.
Kulingana na katibu mtendaji wa tarafa hiyo, amri hiyo iliagizwa yapata miaka miwili iliopita lakini ikapuuzwa.
“Pengine wakati ule sababu ambazo watu hawakupokea vema ujumbe haukuwa umeelezewa sawa sawa ,lakini leo baadhi ya makanisa yalilazimika kufunga milango baada ya kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi huku misikiti yenye vipaza sauti na makanisa yenye kengele tukiyataka kutotumia mtindo huo.
“Mtu aliye lala akiishi jirani na kengele hiyo inampigia kelele. Kwa hiyo ni uamuzi unaohusu pande zote na ni matarajio yetu kuwa hakuna aliyenyimwa haki,” amesema.
Naye mshauri wa Mufti nchini humo, shekh Mbarushimana Suleinam amesema hatua ya kuzuiwa matumizi ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa makanisa na vigango zaidi ya 700 ambavyo viliripotiwa kuwa havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi.
Chanzo:BBC

No comments:

Post a Comment