Friday, 30 March 2018

Urusi yajibu mapigo yawatimua wanadiplomasia 60 wa MarekaniURUSI imewafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani na kufunga ubalozi uliopo St. Petersburg ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi baada ya shutuma ya Uingereza kuhusu kuhusika kwa taifa hilo katika shambulio la jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Kripal na binti yake huko Uingereza.
Sergei Kripal 
Hatua hiyo ilitangazwa na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov. Zaidi ya nchi 20 zimewafukuza wanadiplomasia wa Urusi nchini mwao katika kuunga mkono Uingereza.
Miongoni mwa nchi hizo ni Marekani ambapo mapema wiki hii iliwatimua wanadiplomasia 60 wa Urusi kuondoka Marekani.
Katika kujibu hilo Urusi imewatimua wanadiplomasia 58 kutoka Moscow na wawili kutoka mji wa Yekaterinburg, chombo cha habari cha Interfax kiliripoti. Lavrov amesema nchi nyingine zilizowafukuza Warusi wasubiri majibu kwa vitendo.
Ameongeza kuwa Ubalozi wa Marekani umepewa taarifa kuhusu hatua hiyo kama majibu kwa Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake na kusimamisha ubalozi ulioko St. Petersburg.
Baada ya hatua hiyo msemaji wa Marekani amesema Urusi haina nia ya kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine, na hivyo Marekani ina haki ya kuchukua hatua nyingine dhidi ya Urusi.
''Urusi imeamua kujitenga zaidi yenyewe, tunaangalia uamuzi wa kuchukua'' Heather Nauert amewaambia waandishi wa habari. Urusi imekataa kuhusika kwa namna yoyote na jaribio la mauaji kwa jasusi wake wa zamani.
Kripal bado yupo katika hali mbaya hospitalini lakini binti yake anaendela vizuri na ameondoka katika hali ya hatari.
Urusi imekataa kuhusika kwa namna yoyote na jaribio la mauaji kwa jasusi wake wa zamani.

No comments:

Post a Comment