Monday, 19 March 2018

Utafiti: Upungufu wa mbegu za kiume unahatarisha maishaWanamke na mwanamume wakiangalia matokeo ya ujauzito

WANAUME wenye mbegu chache za kiume wako katika hatari ya kupata magonjwa kulingana na utafiti mpya.
Utafiti uliofanyiwa wanaume 5.177 ulibaini kwamba wenye mbegu chache za kiume wana mafuta mengi mwilini, shinikizo la damu na mafuta machafu katika mishipa ya damu.
Pia wana uwezo mkubwa wa viwango vidogo vya homoni za kiume. Waanzilishi wa utafiti huo wamesema wanaume wenye mbegu chache za kiume pia ni muhimu kufanyiwa vipimo vingine vya magonjwa mengine.
Hivi karibuni hapa nchini kumeshamiri matangazo rasmi na yasiyo rasmi kuhusu dawa asili hususan za kuongeza nguvu za kiume lakini sasa serikali ya imethibitisha matumizi ya dawa tano za asili.
Huku miongoni mwa dawa hizo ni 'Ujana' ambayo kazi yake ni kusaidia kuongeza nguvu za kiume wakati dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na kubaini kuwa hazina madhara kwa afya ya binadamu.
Aidha, Paul Muhame ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa za asili hapa nchini amesema baada ya baraza kupitisha vigezo vyote vilivyohitajika kutoka katika dawa hizo na mamlaka ya dawa na chakula wamethibitisha hilo.
“Suala muhimu ambalo tumeliangalia zaidi ni usalama wa mtumiaji lakini katika upande wa kuthibitisha kuwa dawa hizo zinaponyesha au la, linabaki kwa mnunuaji na mtumiaji wa dawa hiyo,”amesema Muhame.
Upungufu wa mbegu za kiume na matatizo ya ubora wake ni masuala yanayoathiri mmoja kati ya wanandoa watatu kushika mimba kulingana na utafiti huo uliofanywa nchini Uingereza.
Lakini katika utafiti huu mpya wanasayansi walichanganua wanandoa wasioweza kupata watoto nchini Itali kujua iwapo ubora wa mbegu hizo pia unaathiri afya ya mtu kwa jumla.
Waligundua kwamba wanaume wengi walio na mbegu chache walikuwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo mwili ulionenepa na shinikizo la damu.
Hatua hiyo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo na kiharusi.
Wanaume hao pia walionekana kuwa na viwango vya juu vya kuwa na homoni chache za kiume ambazo hupunguza ukubwa wa misuli na mifupa na huenda vikasababisha ugonjwa wa kudhoofika kwa mifupa.
Daktari Albert Ferlin ambaye aliongoza utafiti huo , anasema: Wanaume wasio na rutuba hukumbwa na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuhatarisha hali yao ya maisha na kupunguza kiwango cha maisha wanayoishi.
“Rutuba huwapatia wanaume fursa isiyo ya kawaida ya kutathmini afya na kuzuia magonjwa,”amesema.
Hata hivyo, wamiliki wa utafiti huo wamesisitiza kuwa haukuthibitisha kuwa ukosefu wa mbegu za kiume za kutosha husababisha matatizo ya kimetaboliki lakini badala yake ni vitu viwili vinavyohusiana.
Wanasema uhaba wa homini za kiume huhusishwa na matatizo haya ya kiafya. Dk. Ferlin amesema utafiti unaonesha kwamba ni muhimu kwa wanaume wanaotibiwa matatizo ya ukosefu wa rutuba wanafaa kuangaziwa vizuri kimatibabu.
“Wanaume walio na matatizo ya kuwapatia mimba wake zao wanafaa kukaguliwa vizuri na kufuatiliwa na wataalam wao wa rutuba kwa sababu huenda wana viwango vya juu vya kupata maradhi na vifo,” amesema.
Hata hivyo, uthibitisho wa dawa za asili hapa nchini umezua mjadala mkali katika vipindi vya radio nchini hususan upande wa serikali kuthibitisha dawa za nguvu za kiume kuuzwa kihalali .
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment