Friday, 16 March 2018

Uzinduzi wa vituo mwendo sita vya polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituo hivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo likiwa vitumike katika maeneo ya mkoa huo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Tukio hilo lilifanyika jana Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu. 
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu.

Askari wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi kutoka Mkoa wa kipolisi Kinondoni, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu.

Moja ya Vituo Mwendo vya Polisi vilivyozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), ambavyo vitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia na kupambana na uhalifu.

No comments:

Post a Comment