Friday, 30 March 2018

Viongozi Chadema wapewa dhamana
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Kisutu imetoa masharti ya dhamana kwa viongozi 6 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wawe na wadhamini 2 kila mshtakiwa atakayesaini bondi ya sh. milioni 20.

Pia wadhamini hao wawe na barua za utambulisho, ambapo baada ya kutimizwa masharti hayo, Mbowe na wenzake wawe wanaripoti Polisi Kati (Central Police) mara moja kila wiki.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi ameieleza mahakama ya Kisutu kuwa watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo wa kutoa dhamana dhidi ya Mbowe na wenzake.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka manane likiwemo la kufanya uasi linalomkabili mwenyekiti huyo wa Chadema. Hawakufikishwa mahakamani jana kwa kukosekana gari la mahabusi.

No comments:

Post a Comment