Sunday, 25 March 2018

Viongozi wakuu Chadema washiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi (Mitende) kwenye Kanisa la KKKT, Azania Front Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasssa, leo wameshiriki ibada ya Jumapili ya Matawi kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Dar es salaam.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasssa mwenye koti nyeusi na tai rangi ya damu ya mzee akiwa katika maandamano na waamini wengine kuingia kwenye Kanisa la KKKT Azani Front leo, kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi (Mitende).Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni , Freeman Mbowe akiwa katika Ibada ya Mitende leo (Machi 25, 2018) kwenye Kanisa Kuu la KKKT Azani Front.Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasssa, mwenye nywele nyeupe akishiriki Ibada ya Jumapili ya Mitende kwenye la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front leo Dar es Salaam.

Ibada ya Jumapili ya Matawi huadhimishwa wiki moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka.

No comments:

Post a Comment